MWINGILIANO WA UTANZU WA MODERN TAARABU- MIPASHO NA MAIGIZO

Mwingiliano wa Utanzu Modern Taarabu- Mipasho na Maigizo

Authors

  • Jackline Njeri Murimi a:1:{s:5:"en_US";s:28:"Tom Mboya University College";}

DOI:

https://doi.org/10.14738/assrj.81.9604

Keywords:

Mwingilianotanzu; Mwingilianomatini; Taarab; Modern Taarab; mipasho; maigizo

Abstract

Muziki wa taarab umepata mabadiliko makubwa na kusababisha kuwepo kwa aina mbili kuu za Taarab: Taarab Asili na Modern Taarab.Utafiti huu ulihakiki mwingiliano tanzu katika Taarab-Mipasho. Malengo ya Makala hii yalikuwa ni  kuchanganua miktadha mbalimbali ya mwingiliano tanzu katika muziki wa Taarab ya Mipasho  na utanzu wa maigizo na kutathmini dhima ya mwingiliano huo katika muziki wa Taarab ya Mipasho. Makala hii iliongozwa na nadharia ya mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva (1960) baada ya kuizua kutokana na nadharia ya Mikhail Bakhtin ya Usemezano ambapo imetumika kushughulikia mwingiliano tanzu katika Taarab-Mipasho. Pia nadharia hii imetumika katika kufafanulia uhuru na ubunifu wa mtunzi wa kuingiza vipengele vipya katika kazi. Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo. Ukusanyaji data ulihusisha usikilizaji, utazamaji na unukuzi daftarini wa nyimbo za Taarab ya Mipasho ili kupata mistari, vifungu vya maneno na stanza zilizobainisha mwingiliano tanzu. Sampuli ya utafiti ilikuwa nyimbo 32 za muziki wa Taarab ya Mipasho ambazo ziliteuliwa kumaksudi. Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulitolewa kwa njia ya maelezo ya kina yaliyohusisha udondoaji na ufafanuzi wa mistari, vifungu vya maneno na stanza zenye kudhihirisha mwingiliano tanzu kutoka kwa data asili. Kutokana na matokeo ya utafiti, mwingilianotanzu mkubwa ulibainika katika uwasilishaji wa muziki wa Modern Taarab ya Mipasho uliorejelewa. Utafiti huu unawachochea wahahakiki wengine wa fasihi simulizi katika kufanya uchunguzi zaidi katika mitindo mingine ya nyimbo za modern taarab kwa misingi ya nadharia mbalimbali za fasihi. Aidha, kutokana na utafiti huu, ilitarajiwa kuwa watafiti wataweza kulinganisha na kulinganua mitindo tofauti ya taarab. Hatimaye, mtafiti anapendekeza tafiti zaidi zifanywe ili miongoni mwa mengine, kusuluhisha mgogoro kuhusu taarab ya mipasho, uwezekano wa kujumuisha nyimbo za taarab miongoni mwa vipera vya utanzu wa nyimbo katika awamu zote za usomi na uhakiki wa fasihi simulizi kwani muziki wa taarab na hasa mipasho bado unahitaji utafiti Zaidi.

References

MAREJELEO
Bakhtin, M.M. (1981). The Dialogic Imagination: Four Essays. Ed. Michael Holquist. Trans. Caryl Emerson and Michael Holquist. Austin and London: University of Texas Press.
Muiruri, P. K. (2006). Maandalizi Mufti ya K.C.S.E Fasihi Simulizi, Maswali na Majibu. Palco Enterprises Ltd.
Mulokozi, M. M. (1989). Tanzu za Fasihi Simulizi. Katika, Mulika. Na. 21. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
Mpenzi Chocolate-Mzee Yusuf
1. Utangulizi;
2. Imefika siku yenu, nyie kuwaambia kweli,
3. Huo unafiki wenu, na huo ufedhuli,
4. Hatuachani kwa maneno yenu, labda pindijalali,
5. Endeleeni na mirundo,
6. Sie tumependana,
7. Yeye ndio chocolati wangu, na mimi kwake kali,
8. Moyoni adhiti wangu, anayenificha baridi kali,

9. Basi naukweli, nakutamani wewe,
10. Unifiche baridi, mwili joto uwe,
11. Unaponukia udi, malaika hunisimama mie,
12. Hamu hamu hizi, hebu nikumbatie

13. Poleni nyie mafisadi, au wenye roho za ukaidi,
14. Yeye ndio wa uwaridi,raha zake kwangu huzidi,
15. Ananipa raha, ananipa raha ndani ya roho,
16. Nawapa karaha, nawapa karaha munaumwa roho,

17. Meseji zenu zenu zenu za karaha, Mie hazi, hazi nirushi roho,
18. Hamtaki sisi tule raha,tutazidi kuwaumiza roho
19. Kiwe kimoto ananipulizia,nikiwa na joto ananipepea,
20. Mzigo mzito huja kunitua, enye koroto ananifulia
21. Ye ndio kila kitu kwangu, mpenzi chocolate,
22. Ye ndio binti wangu sisikizi yoyote,
23. Kama ni tamu,
24. Nairamba, alivyotia,
25. Kama ni hamu,
26. Naipenda , aniswabilia
27. Ananitia nakshi, nakshi mahamumu,
28. Kumwacha sitaki, nitajidhulumu.
29. Kidonda tamu nzi ndo hufia,
30. Hapa patamu ndio maana nimetulia
31. Dhahari wazimu japari nimevua
32. Ananitia akshi, akshi mahamumu,

33. Kumwacha sitaki, nitajidhulumu.
34. Wanatamani tuachane,
35. wapi, shanshuu, Tuacheni tulale,
36. Na raha tuzile,
37. Ananitia akshi, akshi mahamumu,
38. Kumwacha sitaki, nitajidhulumu.
39. Halua, halua,
40. Halua, halua,
41. Halua, halua,
42. Halua, halua,
43. Halua halua,halua,
44. Halua, halua,
45. Haya ukitaka halua we chukua,
46. Halua, halua,
47. Ukitaka na tende pia chukua,
48. Halua halua

49. Uchungu moyoni unaniuwa,
50. Halua halua
51. Halua halua,halua,
52. Halua, halua,
53. Nakuona tu, unanifuatilia,
54. Mi nakuona tu, unaning’ang’ania,
55. Japo sitaki we wanifuatilia,
56. Japo sitaki we waning’ang’ania,
57. Nakuona tu, unanifuatilia,
58. Japo sitaki we waning’ang’ania,
59. Umerogwa wewe mwenzetu, Ulirogwa ama umetumwa,
60. Umerogwa.

61. Nei nei babuji,
62. Chuma chuma dede,
63. Nei babuji,
64. Chuma chuma dede,
65. Chuma, chuma,
66. Chuma chuma dede,
67. Ramaskhe babuji,
68. Chuma chuma dede,

69. Utanibeba leo, umekula hela zangu,
70. We utanibeba leo, umekunywa soda zangu,
71. Utanibeba leo, umekula hela zangu sana,
72. We utanibeba leo, siondoki peke yangu,
73. Utanibeba leo, umekula hela zangu,

74. Maneno maneno, mimi siwezi,
75. Kubishana bishana ovyo siwezi,
76. Kugombana gombana ovyo siwezi,
77. Kubishana bishana ovyo siwezi,
78. Nachokiweza labda ni kazi,

79. Hapo chacha,
80. Mimi ninasema ukweli,
81. Hapo chacha
82. Kimya wewe,
83. Helua, helua,
84. Helua, helua,
85. Helua, helua,
86. Haya ukitaka halua we chukua,

87. Halua, halua,
88. Ukitaka na tende pia chukua,
89. Halua halua
90. Haya ukitaka halua we chukua,
91. Halua, halua,
92. Uchungu moyoni unaniuwa,
93. Halua halua

94. Wanaonipenda wanipende,
95. Wanaonichukia na waende zao,
96. Ala, mpende akupendaye,
97. Asokupenda mtimue,
98. Mpende akupendaye, asokupenda usimng’ang’anie
99. Mpende akupendaye
100. Asokupenda mtimue,
101. Mpende akupendaye, asokupenda achana naye
102. Mpende akupendaye
103. Asokupenda mtimue,

104. Mpende akupendaye, asokupenda usimng’ang’anie
105. Mpende akupendayeasokupenda mtimue,
106. Haraka haraka haraka aende kule,Asije akakuua bure.

107. Halua halua, halua halua,
108. Haya ukitaka halua we chukua,
109. Halua, halua,Ukitaka na tende pia chukua,
110. Halua halua
111. Haya ukitaka halua we chukua,
112. Halua, halua,
113. Uchungu moyoni unaniuwa,
114. Halua halua


Full Stop-Khadija Kopa
Utangulizi;
1. Hamisi Simba, mwana nyamala, waambiena kuja.
2. Wamekataa corner wanakubali penalty.
3. kwa mara nyingine tena,
4. Mimi ni mtu wa watu, nisojua kunong’ona.
5. Jamani mapaparazi, mtajuta kuniona mnaingilia mapenzi,
6. Unayopeana na bwana mlianza na mizizi,
7. Penzi si la mwaka jana, hatukuingia juzijuzi jiji la Dar-es-Salama.
8. Umenipandia ngazi, ukashuka na milima.
9. Umelipiga mapenzi, joto joto lazizima.

10. Atayejitia bazazi
11. Ajue hana usalama.
12. Nitamfungia kazi,
13. Na mji atauhama
14. pamoja salamu klabu.
15. Twendekazi.
16. Fullstop wote kimya, zubaisha king’ori naongea.
17. Fullstop acheni kelele, na si rukhsa kujitetea.

18. Ole wenu mnaopita, njia za panya kunifuatilia.
19. Mimi niko majoha mando wa kike, hala ntawaarifu aaah!
20. Tena nalipa, Bishufi wa ukweli,
21. na nnajua kunengua.Kanipenda, kanizimikia ukweli,
22. nahasa pale, naporembua.

23. Sasa wezi wa mabwana, nawaambia mtawachwa katwaa.
24. Nawapa onyo ‘full stop’, hii ni challenge full gear.
25. Nyie, taipu zenu za vichochoroni, ndio zinazowafaa.
26. Sio wangu mimi, chumba na varanda tena ghorofani nampandia.

27. Fullstop jipangeni upya, hapa kwangu mumechemka.
28. Nina ladha tamu sana, ndio maana hataki kutoka.
29. Hata mje na waganga lori nzima, himaya yangu keshafika.
30. Mnilie mizimu na makafara, na mchinje hata paka.

31. ‘Full stop’ jipangeni upya, hapa kwangu mmechemka.
32. Nina ladha sweeti sana, ndio maana hataki kutoka.
33. Hata mje na waganga lori nzima, himaya yangu keshafika.
34. Mnilie mizimu na makafara, na mchinje hata paka.

35. Halafu wajifanya unalipa, hutafuti wako ukamweka.
36. Wewe huezi miliki yangu, baby cute wa Kiafrika.
37. Kwanza mimi niko peke yangu, nimetulia sina shaka.
38. Nimetulia na mume wangu, mtoto wa uhakika.

39. Vikarolaiti vyenu, vinavyowapa jeuri,
40. Hivyo vikarolaiti vyenu, nitavipiga marufuku hapa.
41. Mimi nina rangi yangu, sitaki uso wa baka.
42. Mimi nina rangi yangu,na tena bado nawaka.

43. Bandika bandika, mimi nabandua.
44. Nikuhidi maarifa, huna unalolijua.
45. Bandika bandika, mimi nabandua.
46. Tumependana wawili, wewe unajijua.
47. Hakutaki pesa mbili, hulijui takataka.
48. Bandikabandika, mimininabandua.
49. Bandikabandika, mimininabandua.

50. Semasema, Musa Musa. Musa mipango.
51. Mfalme wabesi Tanzania.
52. Wametoka kwa Harita .

53. Tumependa na wenyewe, maneno maneno ya nini.
54. Eti Zera naughty boy, kwani mnataka nini?
55. Sasa ninawaambia kijana yuko makini.
56. Wala hahitaji foja, maximum nikochini.
57. Hahitaji msichana wa jezi, kiwanda anachondani.
58. Anavyotua vifaa, kama yuko Marekani.

59. Kama yuko Marekani.
60. Usigusemoto utapunguza.
61. Napajuahapa Bongo, pameeneavituko.
62. NakujuakuleZeni, kumeeneavituko.
63. Na Mombasa mjini, pameeneavituko.
64. Kina dada wakwambia, mambo nimpambaiko.
65. Kama hujajipodoa, hapa Bongo hunasoko.

66. Hapa Bongo huna soko.
67. nikwelezejehunasoko.
68. Ninakuwekakipupa,nakupasahunasoko.
69. Usigusemoto utapunguza, usigusemotoutapunguza.

70. Na kina dada wa bongo, wakweli wajanjasana
71. Kina dada wa Mombasa, nanyiewajanjasana,
72. Na kina dada waZenji, kwakweli wajanjasana,
73. Mkifikauwanjani, macho mnatazamana.
74. Sasamkitokanje, mnawagobeamabwana.
75. Mnagobeamabwana, mnagobeamabwana.
76. Eeeh usiguse moto, utakuuguza,
77. Eeeh usiguse moto utakuguza.

78. Wapenzi wangu nawapenda, usifikiriutani,
79. I love you so much, usifikiriutani.
80. Nimewamiss, usifikiriutani.
81. Wapenziwangunawapenda, usifikiri utani.
82. Hatamnapochizika, naposimama stejini,
83. Na pale mnapopagawa, napokuwa uwanjani,
84. Mungekuwa embe dodo, ningewala na majani.

85. Ningewala na majani, ningewala na majani.
86. Usigusemoto, utapunguza, usigusemotoutapunguza.
87. Watotowanguwakiume, nisikilizeninyie,
88. Mnaojiitamasharobaro, nisikilizeni.
89. Nyiemabarobaro, nisikilizeni.
90. Nawaambia kina kaka, wanawakewanajua.
91. Pale pana pa utamu, wamepapambamaua,
92. Ukikosa gonorrhea, ukimwiutakuuwa.

93. Ukimwiutakuuwa, ukimwiutakuuwa.
94. Usigusemoto, utapunguza,
95. Usigusemoto, utapunguza.

96. Kimalizio;
97. Totimoto, watuache.
98. Totimoto, tupishetupite.
99. Totimpangomzima,
100. Totimpangomzima.
101. Loliondo kwa babu, sharubaru kapewa kikombe
Akasema nangoja mrija boi.

Utalijua Jiji-Afua Suleiman

Utangulizi;
1. Kazi yako ufisadi Jeuri ngebe na nongwa
2. Baraka ya ukaidi Ukali kama embe ngwangwa
3. Vituko vya makusudi Si bure we umerogwa
4. Badala ya soda baridi Ama juice ya chungwa
5. Ushamba umekuzidi Andazi wanywia togwa
6. Mwenzangu huna ujuzi Mpenzi umemuudhi
7. Kaja kwangu nimempokea.

8. Pokea chako kibomu Shoga nakutumia
9. Hata ukinilaumu Wako nishamchukua
10. Penzi ulimdhulumu Visa ukamfanyia
11. Chachandu vitamtamu Bwana hukumpatia
12. Bwana kapata wazimu Kashindwa kuvumilia

13. Kwangu akatia timu Tiba nikampatia
14. Nikampa vitu adimu Kwako hajajionea
15. Amri akasalimu Magoti kunipigia
16. Huku akijilaumu Kwako kapotea njia

17. Kapenda yangu nidhamu Na utulivu nyumbani
18. Pamoja na ukarimu Kwa ndugu na majirani
19. Ucheshi na tabasamu Kanijalia manani
20. Nimepewa lugha tamu Nyoka hutoka pangoni
21. Sifa hizi ni muhimu Na mengi mengine ndani
22. Wewe mkaanga sumu Kwako hazipatikani
23. Na mapishi yako bomu Kitimutimu jikoni
24. Wali wautia ndimu Hayo ni mapishi gani
25. Bwana imemwisha hamu Katimua nyumbani

26. Unaningoja njiani Madhila kunifanyia
27. Usitake ushindani Hunishindi nakwambia
28. Mimi naletewa ndani Wewe watanga na njia
29. Magomeni BuguruniNdala za kukatikia
30. Wasela wa vijiweniNafuu wajipatia
31. Uroda kwa foleni Kwako wajipendelea
32. Wewe gumzo mjini Watu wanahadithia
33. Umeachika ndoa niniKwa yako mbaya tabia
34. Unaogea jikoni Bafuni unapikia

35. Kwako kaachia ngazi Kwangu kaweka makazi
36. Sasa akaa mbalizi Kachoka yako maudhi
37. Utamaliza mizizi Waganga na waganguzi
38. Talasimu na hirizi Ongeza na vipodozi
39. Kwake hupati nafasi Mimi ndio yake pumzi

40. Sasa ndo utalijua jiji mwenzangu
41. Chajio utakunywa uji mwenzangu
42. Na juice utakunywa maji mwenzangu
43. Huyu kwako harudi tena mwenzangu
44. Najinafasi najinafasi
45. Utajiju wewe utajiju
46. Kwako nishamchukua Kwako harudi tena we mwenzangu
47. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua
48. Katamka waziwazi Kuwa hakutaki tena we mwenzangu
49. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua
50. Bwana kanipa nafasi Nimuonyeshe ujuzi we mwenzangu
51. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua
52. Nami sifanyi ajizi Mpenzi namuenzi we mwenzangu
53. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua
54. Nampikia maandazi Na chai ya tangawizi we mwenzangu
55. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua
56. Wali wa nazi kwa ndizi Mavitus kama kazi mwenzangu we mwenzangu
57. ohh utalia mwenzangu jiiu utalijua
58. Mwisho natoa dozi Impayo usingizi we mwenzangu
59. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua
60. Mwenzangu huna ujuzi Rudi tena kajifunze we mwenzangu
61. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua
62. Bibi acha upuuzi Kuishi na mume kazi we mwenzangu
63. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua
64. Mume ataka malezi Sio mambo ya kihuni we mwenzangu
65. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua
66. Ngebe na jeuri zako Leo zimekuishia we mwenzangu
67. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua
68. ohh utalia mwenzangu jiji utalijua wee


Umejuaje Kama Si Umbea- Mwanaidi Shaaban
1. Utangulizi;
2. Umejuaje*3
3. Umejuaje nimefanikiwa umejuaje?
4. Umejuaje ukaonafi umejuaje?
5. Umejuaje kama si umbea umejuaje?

6. Umeyatafuta, umeshayapata, sasa walialia
7. Vizurivyakupita, wavikodolea macho,
8. Vinono vykupita wavikodolea macho
9. Vitamu vyakupita wavikodolea macho
10. Wakufuma tumefuma, fuma,wakukosa umekosa, kosa
11. Swadakta, umepata swadakta,
12. Swadakta, nimefanikiwa swadakta,

13. Umesikika waamba, wewe bado unagomba, lipi likusumbualo jambo?
14. Macho yako kama mamba, wala hujui kufumba, hakikupiti kitu kirembo,
15. Japo mie sijatamba,wala sio wa kujigamba,lakini sifichi langu pambo,
16. Kasirika sasa vimba, bure jua hutaziba, wewe jifunze ujue mambo.
17. Endelea kunichimba, nenda kwa wachawi omba, jua Mungu hapigi kwa fimbo,
18. Adabu yako elewa, nimefanikiwa mie,

19. Kiitikio;
20. Jahaza yako elewa nimefanikiwa mie
21. Nimeongokewa mie,
22. Nimejaliwa mie,
23. Unaona fi,kuniona mie kung’aa,
24. Siachi*4, kuvaa mie siachi.
25. Unaona fi,mie kupanda Rav.4 ,
26. Siachi*4, kupanda Rav4 siachi.
27. Unaona fihi,mie kuenda melody ,
28. Siachi, kuenda melody siachi.
29. Wataka kuliziba jua na ungo,
30. Huwezi kuliziba jua,
31. huwezi kuliziba na ungo,
32. Huwezi kuliziba jua,
33. Huwezi kuliziba.

34. Milango uliyofunga, gonga misumari gonga, fanya ukuta ujenge pia,
35. Weka mtu wa kuchunga, hutaniona kusonga, sasa Mungu kanifungulia,
36. Ulie ukining’ong’a, ati mi wa moja kanga, hali ishanibadilikia,
37. Jahazi kutoka Manga, kwangu limetia nanga, neema sasa nailalia.
38. Hebu domo lako funga, kwangu mimi hutachonga, jua Mungu, ameshanilipia

39. Kiitikio;
40. Jaza yako elewa, nimefanikiwa mie,
41. Nimeongokewa mie, nimejaliwa mie.
42. Unaona fi, uliona mie kung’aa,
43. Siachi, kung’ aa mie siachi.
44. Unaona fi,mie kupanda Rav4 ,
45. Siachi, kupanda Rav4 siachi.
46. Unaona fi,mie kuenda melody ,
47. Siachi, kuenda melody siachi.
48. Wataka kuliziba jua na umbo,
49. Huwezi kuliba jua, huwezi kuliziba na umbo,
50. Huwezi kuliziba jua, huwezi kuliziba.

51. Kimalizio;
52. Kalichagua goma, la Kiswahili goma,
53. Chakacha namchezea, habibi namchezea
54. Lele mama namchezea, habibi namchezea
55. Msewe namchezea, habibi namchezea,
56. Hatakibiriani yako, kalichagua bada langu.
57. Sima ya bada hujui kusonga, hujui kusonga sima ya bada.
58. Sima ya bada tamu,
59. ipate mpishi timamu.
60. Ipate papa adhimu,
61. Utie na tui gumu,
62. Pia chachandu ya ndimu
63. Ukilahuishi hamu, huishi hamu kuila.

Downloads

Published

2021-01-24

How to Cite

Murimi, J. N. (2021). MWINGILIANO WA UTANZU WA MODERN TAARABU- MIPASHO NA MAIGIZO: Mwingiliano wa Utanzu Modern Taarabu- Mipasho na Maigizo. Advances in Social Sciences Research Journal, 8(1), 186–197. https://doi.org/10.14738/assrj.81.9604